BOIPLUS SPORTS BLOG

HARARE, Zimbabwe
TIMU ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imekubali kichapo cha mabao 3-0 toka kwa Zimbabwe katika mchezo wa kirafiki wa Kimataifa uliochezwa jioni ya leo jijini humo. Mechi hiyo ipo kwenye kalenda 
Shirikisho la Soka la kimataifa (FIFA)

Mshambuliaji Knowledge Musona anayekipiga katika timu ya KV Oostende ya Ubelgiji ndiye aliyefunga bao la kwanza dakika ya tisa baada ya mabeki wa Stars kuweka mtego wa kuotea na kwenda mapumziko wenyeji wakiwa mbele kwa bao hilo.

Kipindi cha pili Zimbabwe walirudi kwa kasi na kufunga mabao mawili ya haraka haraka dakika za 55 na 57 kupitia kwa Nyasha Mushekwi na Mathew Rusike baada ya ngome ya Stars iliyokuwa chini ya Erasto Nyoni na Vicent Andrew kushindwa kuhimili kashikashi hizo.

Stars haikuwa na muunganiko mzuri kiuchezaji katika mchezo huo ambapo Zimbabwe walikuwa na uwezo wa kupata mabao zaidi hasa kipindi cha pili kutokana na mashambulizi yao waliyofanya langoni mwa vijana wa Kocha Charles Mkwasa ambapo wangeweza kupata kipigo cha aibu.

Matokeo hayo yanategemea kuendelea kuishusha zaidi Tanzania kwenye viwango vya FIFA vinavyotolewa kila mwezi ambao kwa sasa ipo nafasi 144.

Post a Comment

 
Top