BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
MSHAMBULIAJI Jerson Tegete amefunga mabao mawili lakini yameshindwa kuinusuru timu yake ya Mwadui kupokea kichapo cha mabao 3-2 dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Mwadui Complex.

Tegete aliyetokea benchi alifunga mabao hayo dakika ya 63 kwa mpira wa adhabu karibu kabisa na lango la Mtibwa huku lile la pili akitupia dakika ya 93 baada ya kumzidi ujanja golikipa Saidi Mohamed 'Nduda'.

Haruna Chanongo ndiye aliyefungua karamu hiyo ya mabao kwa upande wa Mtibwa katika dakika ya sita kabla ya Kelvin Friday na Rashidi Mandawa kuwamaliza 'Wachimbaji' hao wa madini ya Almasi.

Mwamuzi Jonesia Rukyaa alimtoa kwa kadi nyekundu Mandawa baada ya kupoteza muda makusudi dakika ya 74 na kuwafanya Wakata miwa hao wamalize pungufu katika robo ya mwisho ya mchezo huo.

Mchezo mwingine uliopigwa leo hii Kagera Sugar iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbao FC na kufikisha alama 21 na kupaa hadi nafasi ya nne.

Post a Comment

 
Top