BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
TIMU ya Taifa ya Wanawake 'Twiga Stars' itasafiri Novemba 8 kuelekea nchini Cameroon kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa Kimataifa utakaofanyika nchini humo kwa ajili ya kuziweka sawa timu zote.

Shirikisho la Mpira la mpira wa miguu la Cameroon (CFF) liliiandikia barua TFF kuhitaji kucheza mechi ya kirafiki kutokana na kiwango cha juu kilichoonyeshwa na Twiga hasa baada ya kuchukua ubingwa wa Afrika Mashariki na kati  mashindano yaliyofanyika nchini Uganda mwezi Septemba.

Kikosi cha Twiga kimeshaingia kambini kwenye Hostel za TFF ambapo Kocha Sebastian Mkoma amekuwa na programu za mazoezi kulingana na nafasi ya Uwanja wa Karume kutokana na mechi za ligi daraja la kwanza na Serengeti boys ambao pia wanatumia dimba hilo.

Ofisa Habari wa TFF Alfred Lucas alisema kuwa maandalizi kuelekea mchezo huo yamekamilika na timu hiyo itasafiri Jumanne ijayo tayari kwa mtanange huo.

"Kila kitu kinaenda kama kilivyopangwa timu ya Twiga imepata mwaliko toka nchini Cameroon na maandalizi yake yamekamilika ambapo itasafiri Jumanne ijayo," alisema Lucas.

Lucas alisema pia siku hiyo timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys nayo itasafiri kuelekea Korea Kusini kwa ajili ya michuano maalum itakayofanyika nchini humo ambayo Tanzania imealikwa.

Post a Comment

 
Top