BOIPLUS SPORTS BLOG

LONDON, Uingereza
TIMU ya Taifa ya Uingereza 'Three Lions' imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Scotland kwenye mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la dunia litakalofanyika nchini Urusi mwaka 2018 mtanange uliopigwa Uwanja wa Wembley.

Wachezaji wawili wa timu ya Liverpool Daniel Sturridge na Adam Lallana waliwafanya wenyeji kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao mawili baada ya kila mmoja kufunga bao.

Beki wa kati Gary Cahill aliifungia Uingereza bao la tatu dakika ya 61 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na nahodha Wayne Rooney.

Katika michezo huo uliokuwa wa upande mmoja Uingereza ingeweza kupata mabao mengi zaidi lakini umakini katika umaliziaji ulikuwa tatizo ambapo winga Rahim Sterling alipoteza nafasi kadhaa za wazi.

Mchezo mwingine mwingine mchezaji wa zamani wa Arsenal anayekipiga Werder Bremen Serge Gnabry alifunga hat trick akiisaidia Ujerumani kuibuka na ushindi wa mabao 8-0 dhidi ya San Marino ugenini katika mechi ambayo wageni walitawala kila Idara.

Matokeo mengine ya mechi za kufuzu zilizopigwa

Ufaransa 2-1 Sweden
Czech       2-1 Norway
N. Ireland 4-0 Azerbaijan
Armenia   3-2 Montenegro
Denmark  4-1 Kazakhstan
Romania   0-3 Poland
Malta         0-1 Slovenia
Slovakia    4-0 Lithuania

Post a Comment

 
Top