BOIPLUS SPORTS BLOG

KHARTOUM, Sudan
BEKI wa zamani wa timu ya Azam raia wa Ivory Coast Segre Pascal Wawa amesaini mkataba wa miaka miwili na timu yake ya zamani ya Al Merreikh ya Sudan.

Wawa alijiunga na Azam akitokea Merreikh mwaka 2014 baada ya kuisaidia timu yake kunyakua ubingwa wa Kombe la Kagame lililochezwa nchini Rwanda ambapo kwenye mchezo wa Fainali waliwafunga APR bao 1-0.Beki huyo kisiki hakutumika sana kwenye kikosi cha Kocha mhispania Zeben Hernandez kutokana na kuwa majeruhi lakini taarifa zinadai hakukuwa na maelewano mazuri na benchi la ufundi.

Wawa alikuwa miongoni mwa wachezaji tegemeo kwenye kikosi cha Azam chini ya Kocha Stewart Hall msimu uliopita kabla maisha hayajabadilika baada ya kuwasili kwa Mhispania Hernandez.

Post a Comment

 
Top