BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu  

MOURINHO: MESSI BAKI BARCELONA
KOCHA mkuu wa Manchester United Mreno Jose Mourinho ametoa maoni yake juu ya tetesi zilitokea karibuni kuwa huenda mshambuliaji Lionel Messi akaihama klabu yake Barcelona.

Kumekua na tetesi kuwa klabu za jiji la Manchester  zinafuatilia suala la mkataba mpya wa Messi ili kuangalia uwezekano wa kumpata mbambuliaji huyo raia wa Argentina anayetarajiwa kusaini mkataba mpya kabla msimu haujaisha

Mourinho alisema "kila msimu habari zimekua zile zile kuwa Messi anaondoka Barcelona, ila ninavyoona itakuwa vyema kama Messi atabakia katika klabu yake na kustaafia hapo, anastahili kuwepo pale na ndio maoni yangu."STURRIDGE KUTIMKA LIVERPOOL  

MSHAMBULIAJI wa Liverpool Daniel Sturridge anafikiria kuwakacha majogoo hao wa Anfield baada ya nafasi yake kuwa mashakani kufuatia kutopata namba kwenye kikosi cha kwanza na kuwafanya Southampton kujiandaa kutoa ofa ya   paundi  25 milioni kwa Muingereza huyo.

Nafasi yake imekua ya mashaka kutokana kocha Jurgen Klopp kuwatumia zaidi Sadio Mane, Roberto Firmino na Phillipe Coutinho katika nafasi za ushambuliaji huku akimuacha Sturridge kama mchezaji wa akiba

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea huenda akafikiria nafasi yake ya kuitwa timu ya taifa katika Fainali za kombe la dunia 2018 zitakazofanyika nchini Urusi kama hatoendelea kupata nafasi klabuni hapo.COSTA NA COURTOIS KUSAINI MIKATABA MIPYA CHELSEA  

UHUSIANO wa kocha wa Chelsea Antonio Conte na wachezaji wake unazaa matunda baada ya kupata matokeo mazuri na kufanya wachezaji waliotazamiwa kutimka klabuni hapo Diego Costa na kipa Thibaut Courtis kukubali kusaini mikataba mipya.

Wachezaji hao walikua mbioni kutimka baada ya kutokuwa na mahusiano mazuri na kocha wao wa zamani Jose Mourinho ambae alipelekea klabu kufanya vibaya na kumaliza nafasi mbaya katika ligi isiyozoeleka

Costa huenda akapandishiwa dau kutoka paundi 150,000 kwa wiki hadi paundi 200,000 huku Courtois akipandishiwa kutoka  paundi 100,000 kwa wiki  hadi kufikia paundi 150,000.

Post a Comment

 
Top