BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu

BAUZA:MESSI HANIPANGII KIKOSI
KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Argentina Edgardo Bauza amekanusha uvumi wa kwamba nahodha wa timu hiyo anayechezea  Barcelona Lionel Messi anahusika katika kufanya maamuzi ya upangaji wa kikosi cha Taifa hilo.

Kocha huyo  aliiambia DeporTea. "wanasema kwamba Messi anachagua marafiki zake kuwepo katika kikosi cha Argentina ni uongo mtupu, uvumi huu unaletwa na vyombo vya habari."

Messi amehusishwa na kusababisha kutoitwa kwa Ezekiel Lavezzi na Mauro Icardi ambaye inasemekana alimchukulia mwanamke rafiki wa Messi, Maxi Lopez hivyo kupelekea Messi kutopenda kuwepo katika timu hiyo ya Taifa.RONALDO: GRIEZMANN ANANICHUKIA
CRISTIANO Ronaldo baada ya fainali ya mataifa barani ulaya, alienda likizo Miami akakutana na Antoine Griezmann katika mgahawa aliokuwa akipata chakula cha jioni na mchumba wake ambapo mshambuliaji huyo wa Atletico Madrid alimtamkia wazi wazi kuwa anamchukia.
"Griezmann alikuja juu ya meza yangu na alisema kwa tabasamu,  Cristiano nakuchukia".

Griezmann alishindwa kuzuia hisia zake  kutokana na matokeo mabaya katika mashindano makubwa Ulaya ikiwa ni kufungwa na Ureno katika fainali za mataifa barani humo akiwa na Ufaransa na kupoteza pia ubingwa wa ligi ya mabingwa akiwa na Atletico Madrid mjini Milan wakifungwa na Real Madrid anayochezea Ronaldo.

Mshambuliaji huyo  huenda akaendelea kumchukia zaidi Ronaldo  baada ya kufunga 'Hat trick' dhidi ya Atletico katika mechi iliowakutanisha pale Vicente Calderon katika kichapo cha 3-0 wiki iliyopita.MOURINHO: MKHITARYAN HAYUPO TAYARI KWA MECHI KUBWA
Pamoja na kusajiliwa kwa gharama kubwa ya pesa kiungo Henrik Mkhitaryan amekua hapagwi katika kikosi cha Manchester United katika michezo mbalimbali, Meneja wa Manchester United Jose Mourinho alisema mchezaji hayupo tayari kucheza katika mechi kubwa

Raia huyo wa Armenia amekosa mechi dhidi ya Arsenal iliyofanyika Jumamosi iliyopita ikidhaniwa ni kwasababu kiungo huyo hajawa na ubora ambao kocha Mourinho angemuamini na kumpa nafasi hiyo

Jose Mourinho alinukuliwa akisema
"Nilimwambia, hii mechi ya Arsenal  ilikuwa ni mchezo si kwa ajili yenu, sidhani unahitaji muda wa dakika 10 au 20 kutoka benchi, nadhani unahitaji mchezo mzuri na unahitaji ama kuanza au kama si kuingia katika nusu ya pili"

Mchezaji bora huyo wa ligi ya ujerumani kwa msimu 2015-2016 maarufu kama Bundes Liga amekua hana raha klabuni hapo kutokana na kutopata nafasi ya kutosha na muda mwingi kutumia akiwa benchi.

Post a Comment

 
Top