BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu, Mbeya
YANGA leo imetakata katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya baada ya kuifunga Prisons bao1-0 kwa mkwaju wa penalti iliyopigwa na Simon Msuva dakika ya 74.

Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha pointi 30 ikiwa nyuma ya pointi tano ya Simba amabayo ina pointi 35 baada ya kupoteza mechi na African Lyon kwa bao 1-0, mechi iliyochezwa Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.


Msuva aliipatia Yanga bao hilo baada ya Obrey Chirwa kufanyiwa faulo na James Mwasote hivyo mwamuzi wa mchezo huo Hans Mabena akiamuru ipigwe penalti.


Hadi mapumziko timu hizo ambazo zote zilipoteza mechi zao za awali zilikuwa hazijafungana ingawa  Prisons ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata penati iliyopigwa na Lambert Subianka dakika ya 54 baada ya Deus Kaseke kumchezea rafu 


Victor Hangaya, hata hivyo kipa Beno Kakolanya ambaye ilikuwa ni mechi yake ya kwanza kudaka alidaka penalti hiyo.


Yanga watalazimika kurejea jijini Dar esSalaam kwa ajili ya mechi yao ya mwisho kwa mzunguko huu dhidi ya Ruvu Shooting iliyopoteza mechi yake ya leo kwa kipigo cha bao 3-1 dhidi ya Kagera Sugar, mechi iliyochezwa Uwanja wa Kaitaba. 


Prisons wao wataisubiri Simba ambayo inaondoka kesho  Jumatatu huku mechi yao itachezwa Novemba 10, Alhamisi.


Matokeo mengine;

Mbao 2 - 1 Azam 
Ndanda 2- 1 Stand United
JKT Ruvu 1-1 Toto African

Mechi za kesho

Mtibwa Sugar vs Mbeya City (Manungu)
Mwadui vs Majimaji (Mwadui Complex)

Post a Comment

 
Top