BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
Ally Kiba katikati akiwa na vijana wake walioshika tuzo zake tatu

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Ally Kiba ameng'ara katika tuzo zilizotolewa na kituo cha Runinga cha East Africa Television (EAT AWARDS 2016) zilizofanyika kwa mara ya kwanza nchini kwenye Ukumbi wa Mlimani City usiku wa kuamkia leo baada ya kunyakua tuzo tatu.

Kiba amechukua tuzo ya Mwanamuziki Bora wa mwaka, Video Bora ya mwaka na wimbo bora wa mwaka kwa wimbo wake wa 'Aje' ambapo katika vipengele vyote vitatu alivyoshiriki ameibuka mshindi.

Msanii wa filamu za kibongo Salum Ahmed 'Gabo' ameibuka mshindi kwa upande wa wanaume huku filamu yake aliyocheza ya 'Safari ya Gwalu' ikiibuka filamu bora ya mwaka na Chuchu Hansi amekuwa mshindi kwa wanawake.

Lady Jaydee amechaguliwa kuwa msanii bora wa kike huku Manfongo akichaguliwa mwanamuziki bora chipukizi na Nevy Kenzo likiwa kundi bora la mwaka.

Muandaaji wa muda mrefu wa muziki wa kizazi kipya Boniventure Kilosa 'Bonny Love' amenyakuwa tuzo ya Heshima kwa kuthamini mchango wake baada ya kutumia miaka 31 kuutumikia na kusaidia kufikisha muziki huo hadi ulipo sasa.

Post a Comment

 
Top