BOIPLUS SPORTS BLOG

BASEL,Uswisi

BAADA ya miaka sita hatimaye timu ya Arsenal imeamaliza kinara kwenye kundi katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya baada ya kuifunga FC Basel mabao 4-1 mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa St Jacob Park.

Washika bunduki hao wamemaliza vinara wa kundi A wakiwa na pointi 14 wakifuatiwa na Paris Saint Germain wenye alama 12 baada ya kulazimishwa sare dhidi ya  Ludogorets ya mabao 2-2 ambapo winga Angel Di Maria aliwasawazishia wenyeji dakika za majeruhi.

Mshambuliaji Lucas Perez amefunga 'hat trick' yake ya kwanza tangu asajiliwe na Arsenal akitokea Deportivo La Coruna mwanzoni mwa msimu huu huku kinda Alex Iwobi akimalizia la mwisho dakika ya 54 na lile la kufutia machozi la wenyeji likifungwa na Saydou Doumbia dakika  ya 78.

Licha ya Arsenal kuibuka na ushindi huo mnene lakini mechi haikuwa nyepesi sana kwao kwani wenyeji walijitahidi kufanya mashambulizi hasa alipoingia Doumbia lakini safu ya ulinzi iliyokuwa chini ya Laurent Koscienly na Robby Holding ilikuwa imara.

Matokeo ya mechi nyingine zilizochezwa leo ni 

Benifica 1-2 SSC Napoli
Dynomo Kyiv 6-0 Bekistas
Barcelona 4-0 Borussia Monch'blach
Bayern Munich 1-0 Atletico Madrid
PSV Eindhoven 0-0 FC Rostov

Post a Comment

 
Top