BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar

MKUTANO mkuu wa dharura wa klabu ya Simba umefunguliwa rasmi na Rais Evans Aveva huku wanachama waliohakikiwa na kuingia ukumbini wakiwa ni 642. 

Mkutano huo maalumu kwa ajili ya mabadiliko ya katika ya klabu hiyo unafanyika kwenye ukumbi wa Polisi Officers Mess Osterbay jijini Dar es Salaam.


Hizi hapa ni Ajenda saba za mkutano huo:

1.Uhakiki wa wanachama walio hudhuria mkutano.

2.Kufungua mkutano.

3.Hotuba ya Rais

4.Kusoma na kujadili mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba

5.Kupiga kura mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba

6.Majumuisho ya mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba

7.Kufunga Mkutano.


BOIPLUS imepiga kambi kwenye mkutano huu kwa ajili ya kuwajulisha wasomaji wetu kila kinachoendelea kutoka ukumbini hapa.

Post a Comment

 
Top