BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu, UKEREWE
KITUO cha kulea na kukuza vipaji vya michezo kwa vijana cha Victoria (VIYOSA) kimeandaa mashindano maalumu kwa mchezo wa soka yanayotambulika kama Kombe la Sikukuu ya Krismas (BOIPLUS X-MASS CUP) ambayo yamefunguliwa rasmi leo Jumatatu. 

Michuano hiyo inayoshirikisha timu nane inafanyika katika Uwanja wa Mongela wilayani Ukerewe ambako ndiko makao makuu ya kituo hicho yalipo. Michuano hiyo itakwenda sambamba na utambulisho wa kituo hicho utakaofanyika wakati wa kilele cha mashindano hayo Desemba 26.


Mechi ya ufunguzi ambayo ilizikutanisha timu ya Viyosa ambao pia wanashiriki dhidi ya Namagondo ilimalizika kwa dakika 90 zikiwa zimetoka sare ya bao mbili.
Namagondo ndiyo walikuwa wa kwanza kuliona lango la wenyeji wao katika dakika ya 34 likifungwa na Nicodemus Zabron huku Hamady 'Madizo' akiisawazishia Viyosa dakika ya 41.


Namagondo walifanikiwa kufumua nyavu za wapinzani wao kwa mara ya pili ikiwa ni dakika ya 55 kupitia kwa Boniface Vedastus huku Viyosa nayo ikijibu mapigo dakika ya 86 kupitia kwa mchezaji wao Willy Manumbu.


Mechi hiyo ililazimika kuingia hatua ya penalti ili kumpata mshindi kwani michuano hiyo huchezwa kwa mtindo wa mtoano na ndipo Viyosa iliposhinda kwa penalti 6-5.Meneja wa kituo hicho, Godfrey Mugeta ameiambia BOIPLUS kuwa, "Yatakuwa ni mashindano ya siku saba na yatachezwa kwa mfumo wa mtoano, kutakuwepo na zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi wa tatu.


"Tumeanzisha mashindano haya ambayo fainali zake ni Disemba 25 siku ambayo tutatambulisha pia kituo chetu," alisema Mugeta. 


Mugeta alizitaja timu nyingine kuwa ni Smart Boys, Kagera FC, UDC, Boma na Nantare FC.


Picha zaidi za pambano hilo;

Post a Comment

 
Top