BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu, UKEREWE
TIMU ya Boma FC imetinga fainali ya michuano ya BOIPLUS X-MASS CUP inayoendelea kwenye uwanja wa Mongela visiwani Ukerewe mkoani Mwanza baada ya kuifunga UDC mabao 2-0.

Boma itakutana na Viyosa kwenye mchezo wa fainali ambayo iliifunga kwa mikwaju ya penalti 5-4 timu ya Yosso Disemba 24 huku mtanange huo utapigwa keshokutwa Jumatano.


Dioniz Klavely aliifungia Boma mabao yote mawili dakika ya 27 na 91 na kuisaidia timu yake kutinga fainali ambayo inatarajiwa kuwa ya kukata na shoka kutokana na uimara wa timu zote mbili.

Kesho Jumanne kutakuwa na mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu kati ya Yosso na UDC utakaopigwa kwenye uwanja huo ambao utaanza saa 10 jioni.

Post a Comment

 
Top