BOIPLUS SPORTS BLOG

Sheila Ally
HATIMAYE Mshambuliaji wa Mbeya City, Zahoro Pazzi amepata ITC yake iliyokuwa ikishikiliwa na timu ya FC Lupopo ya DR Congo kwa zaidi ya miaka miwili sasa.

Hivi karibuni Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Jamal Malinzi alikutana na mchezaji huyo baada ya kuelezwa jinsi ITC hiyo ilivyotolewa na shirikisho hilo na kuahidi kulishughulikia ndani ya siku saba.

Malinzi aliwahi kuiambia BOIPLUS kuwa atashughulikia ITC  hiyo na kwamba Zahoro ni lazima acheze mechi za Ligi Kuu Bara kuanzia mzunguko huu wa pili na huenda kocha Kinnah Phiri sasa atamtumia kwenye mechi ijayo dhidi ya Mbao FC itakayochezwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Post a Comment

 
Top