BOIPLUS SPORTS BLOGKarim Boimanda
TIMU ya KRC Genk inayoshiriki ligi kuu nchini Ubelgiji imesitisha mkataba na kocha wake Peter Maes muda mfupi uliopita.

Habari za ndani kutoka klabuni hapo zinasema Uongozi umewatangazia wachezaji juu ya uamuzi huo huku sababu ikielezwa kuwa ni kushuka kwa kiwango cha timu hiyo inayowakilisha nchi kwenye michuano ya kombe la Europa.


Taarifa zaidi zinasema Maes ambaye mkataba wake ulikuwa umalizike mwishoni mwa msimu huu alikataa kuongeza mkataba ikiwa ni ishara kuwa alikuwa ameshapata timu nyingine jambo lililowafanya viongozi wahisi ndicho chanzo cha matokeo mabovu ya timu hiyo.

Maes ameitumikia Genk kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi mitano tu tangu ajiungenao huku mtanzania Mbwana Samatta akiwa ni katika wachezaji wake wa mwanzo kabisa kuwasajili kikosini humo. 

Post a Comment

 
Top