BOIPLUS SPORTS BLOG


Akram Msangi, DAR
DAKIKA chache kabla pambano kati ya JKT Ruvu na Yanga halijaanza, bechi la ufundi la mabingwa hao watetezi limefanya mabadiliko katika kikosi chake ambapo kiungo mpya Justine Zulu 'Mkata Umeme' atalazimika kukaa jukwaani.

Zulu ambaye mapema leo alitajwa kuwemo kwenye orodha ya wachezaji wa akiba atatazama mchezo huo akiwa jukwaa kufuatia kile kilichoelezwa kuwa ni kibali chake cha kazi kutopatikana kwa wakati.

Said Makapu ambaye alikuwa jukwaani amelazimika kuvaa jezi haraka na kwenda kukaa benchi badala ya nyota huyo wa zamani wa Zesco ya Zambia.

Post a Comment

 
Top