BOIPLUS SPORTS BLOG

MANCHESTER, Uingereza
TIMU ya Chelsea imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza baada ya kushinda mabao 3-1 dhidi ya Manchester City mtanange uliopangwa uwanja wa Etihad.

City walienda mapumziko wakiwa mbele kwa bao moja baada ya beki Garry Cahill kujifunga dakika ya 44 katika harakati za kuokoa krosi iliyopigwa na Jesus Navas.


Diego Costa aliisawazishia Chelsea dakika ya 60 baada ya kupokea mpira mrefu uliopigwa na Cesc Fabregas kabla ya kumuhadaa beki John Stones na kupiga shuti la chini lililomshinda golikipa Claudio Bravo.

William alifunga bao la pili dakika ya 70 akipokea pasi ya Costa kabla ya Eden Hazard kumalizia karamu ya magoli dakika ya 90 baada ya kupewa pasi na beki Marcos Alonso.


Mwamuzi Anthony Tylor aliwatoa kwa kadi nyekundu Sergio Aguero na Fernandinho dakika za mwisho baada ya kucheza mchezo usio wa kiungwana kwa David Luiz na Fabregas.

Chelsea wamefikisha pointi 34 baada ya kushuka dimbani mara 14 huku wakipoteza mchezo mmoja tu dhidi ya Arsenal mpaka sasa.

Post a Comment

 
Top