BOIPLUS SPORTS BLOG

Sheila Ally, Dar

KAMA wewe ni mvivu basi unaweza kumchukia kocha mkuu wa Mbeya City, Kinnah Phiri ambaye ameamua kutoa mazoezi magumu kwa wachezaji wake.

Wachezaji wa Mbeya City wamepigishwa kwata kwa siku tatu mfululizo ambapo wamelalamika kuwa mazoezi ni magumu na hawajawahi kupewa mazoezi kama  tangu kocha huyo atue kikosini hapo.

Phiri amesema kuwa ameamua kutoa mazoezi hayo ili kuwajenga ambapo alianza na mazoezi mepesi yaliyokuwa yanafanyika mara moja kwa siku baadaye aliongeza dozi ya mazoezi waliyofanya mara mbili kwa siku huku akitamka kuwa kuanzia kesho Jumanne dozi hiyo itapungua tena.

"Tunaelekea kwenye mechi hivyo nitalazimika kupunguza mazoezi na watafanya mara moja kwa siku na kwa saa mbili na nusu tofauti na sasa ambapo wanafanya zaidi ya masaa hayo.

"Kesho nadhani tutatangaza wachezaji wote tuliowasajili kwenye dirisha dogo maana walikuwepo wengi ila tayari nafasi ambazo nilihitaji kuboresha nimefanya hivyo kupitia hawa wachezaji niliowapendekeza," alisema Phiri.

Akizungumzia mechi ijayo dhidi ya Kagera Sugar, Phiri alisema kuwa, "Itakuwa mechi ngumu ila tunataka tushinde mechi zote tutakazocheza hapa nyumbani maana kuna mechi kama tatu tutakuwa nyumbani,".

Post a Comment

 
Top