BOIPLUS SPORTS BLOG

HUMMELS AMPIGIA DEBE MKHITARYAN UNITED
BEKI wa kati wa Bayern Munich Mats Hummels amemuomba kocha wa Manchester Utd Jose Mourinho kumpa nafasi zaidi kiungo Henrikh Mkhitaryan kwenye kikosi cha kwanza cha Mashetani hao Wekundu.

Hummels aliiambia Daily Mail kuwa  "ukimpa nafasi ya kucheza utaona ni kwa jinsi gani Mkhitaryan alivyo bora nina uhakika asiIimia 100 ni mmoja wa viungo bora niliowahi kucheza nao, niliona sehemu ya mchezo wao dhidi ya Feyenoord na niliona uzuri alionao akiwa dimbani, alicheza hivyo msimu uliopita akiwa Dortmund".

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 ameanza mechi ya pili katika ligi kuu nchini Uingereza baada ya kumfurahsiha  Mourinho katika mechi za ligi Europa dhidi ya Feyenoord na kombe la ligi dhidi ya West Ham United.


GUARDIOLA AWAFARIJI UNITED
Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amewafariji jirani zao Manchester United kuwa wanaweza kumaliza nafasi ya nne pamoja na kutokuwa na matokeo mazuri katika ligi kuu nchini Uingereza.

Muhispania huyo ambaye klabu yake ipo nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu alisema "kwa wanavyocheza sasa bado naamini watamaliza nafasi ya nne niliangalia mechi zao dhidi ya Stoke, Burnley na nyingine pale Old Trafford walistahili kushinda mechi hizo lakini soka ndio lipo hivyo".

Guardiola alisema kuwa United wana wachezaji wazuri na wana historia na makocha wanaoweza kuwapeleka hapo, bado ni safari ndefu kugombania ubingwa na haitokuwa rahisi kutomaliza nafasi ya nne.

Post a Comment

 
Top