BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda
BAADA ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom kusimama kwa mwezi mmoja kupisha usajili wa dirisha dogo, wachezaji mbalimbali walipata nafasi ya kupumzika kabla ligi hiyo haijaanza tena Desemba 17. 

BOIPLUS ilizungumza na baadhi ya nyota wakiwemo wale wanaocheza soka nje ya nchi kujua kile wanachofanya kipindi cha mapumziko.


ANDREW VICENT 'DANTE' (Yanga)
"Nikiwa mapumziko shughuli yangu kubwa ni kulisha mifugo kama mbwa, ng'ombe nk. Lakini baada ya hapo huwa napenda kucheza 'video game' tu na washkaji".


JOSEPH KIMWAGA (Mwadui FC)
"Nakuwa zaidi nyumbani na familia, lakini muda mwingi nafanya mawasiliano na meneja wangu tujue tunafanya nini kuhusu hatma ya maisha yangu ya soka, yeye ni mtu muhimu sana kwangu,".


CLIFF BUYOYA (KMC)
"Napiga matizi ufukweni, kwanza huwa natamani mapumziko yenyewe yaishe tu turudi mzigoni. Nina hasira sana na jezi ya timu ya Taifa"


MBWANA SAMATTA (KRC Genk, Ubelgiji)
"Mwanangu hicho ndio kipindi pekee napata muda mzuri wa kukaa na washkaji, huwa nawaita nyumbani tunacheza 'game' na wakati mwingine natoka nao kwenda mahali tulivu kubadilishana mawazo,".


DITRAM NCHIMBI (Mbeya City)
"Natumia likizo kufuatilia mishe zangu tu hasa masuala ya kilimo. Si unajua kule kwetu Tunduru mambo ya korosho na mpunga, basi hayo ndio mambo yangu nikiwa likizo".


JUMA LUIZIO (Zesco, Zambia)
"Kiukweli huku hata nikipata likizo ndogo lazima nikimbie nyumbani kusalimia familia. Huwa nakaa hapo Dar siku chache halafu naenda Morogoro ambako kuna mashamba, mimi nina bustani ya nyanya, karoti na mbogamboga nyingine kule,".


BENNO KAKOLANYA (Yanga)
"Starehe yangu kubwa ni kutazama movie, yaani nikiwa likizo hiyo ndio shughuli yangu kuu. Zaidi ya hapo huwa ni kusalimia ndugu jamaa na marafiki,".


EMILY MUGETA (Neckarsulm SU, Ujerumani)
"Likizo mimi ni ngumi tu kaka, napenda sana mchezo wa ngumi, kutazama na hata kucheza pia. Wakati mwingine nacheza Rugby. Huku kuna baridi kali mno kwahiyo likizo ni lazima ujishughulishe kwa michezo mingine,".VICENT ANGBAN (Simba)
"Nina familia changa ambayo inahitaji sana upendo wangu, kwahiyo mimi nikipata likizo sina ninalowaza zaidi ya kukimbia kwenda kuburudika na familia yangu,".


HIMID MAO (Azam FC)
"Babu hapa ni 'game' tu mwanzo mwisho, kama uko fit nitembelee siku moja nikufundishe kazi. Kipindi cha likizo ndio wakati angalau mtu unaweza kuangalia mambo yako unayoshindwa kuyasimamia wakati ligi inaendelea, lakini nikitoka huko nafikia kwenye game,".

JEAN MUGIRANEZA 'Migi' (Azam) 
"Kipindi cha likizo tulipewa programu ya kutulia tu bila kufanya chochote hivyo nakuwepo tu nyumbani, tukirudi kwenye timu tutaendelea na ratiba ambayo watatupa,".

Post a Comment

 
Top