BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
KIKOSI cha timu ya Yanga leo kimefanya mazoezi yake ya mwisho kwenye uwanja wa Uhuru na kuonyesha kuwa kiko tayari kwa safari ya kesho kuelekea visiwani  Zanzibar kwenye michuano ya kombe  la Mapinduzi.

Kikosi hicho chini ya kocha George Lwandamina kitaondoka kesho saa tisa alasiri kwa boti katika msafara utaokuwa na wachezaji 26 pamoja na benchi la ufundi huku mechi yao ya kwanza  wakicheza Jumatatu saa 2:30 usiku dhidi ya Jamhuri kwenye  uwanja wa Amani. 


Kikosi kamili cha Yanga kitakachosafiri kesho ni:

Makipa Deogratius Munishi, Beno Kakolanya na Ali Mustafa

Walinzi Nadir Haroub, Pato Ngonyani Vicent Andrew, Hamis Hassan, Mwinyi Haji, Kelvin Yondan, Juma Abdul na Oscar Joshua.

Viungo ni Haruna Niyonzima, Justin Zulu, Simon Msuva, Juma Mahadhi, Geofrey Mwashiuya, Deus Kaseke, Said Juma, Thaban Kamusoko na Yusuph Mhilu.

Washambuliaji ni Donald Ngoma, Amissi Tambwe, Emmanuel Martin Obrey Chirwa na Mateo Anthony. 

Yanga itamkosa beki wake Vicent Bossou aliyekwenda kuiwakilisha nchi ya Togo katika Michuano ya Afrika itakayofanyika nchini Gabon mwezi Januari mwakani.

Post a Comment

 
Top