BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu

KIKOSI cha Maafande wa JKT Ruvu kimejipanga kuharibu sherehe ya Krismas kwa wapenzi na mashabiki wa timu ya Simba kwa kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mchezo wa ligi utakaofanyika keshokutwa Jumamosi.

Mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam ambapo Maafande hao wamejipanga kuharibu kabisa sherehe hiyo kwakua hakuna njia nyingine kwa Wekundu hao kuepuka kichacho.

Ruvu wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa mabingwa watetezi Yanga wikiendi iliyopita sasa wamedhamiria kuamka kwa watani wao Simba ambao ndiyo wanaongoza ligi wakiwa na pointi 38 baada ya kuifunga Ndanda FC mabao 2-0 ugenini.


Maafande hao wanaendelea kujinoa kwenye viwanja vya JKT Mbweni chini ya Kocha mkuu Bakari Shime wakiwa na lengo moja la kuhakikisha wanaondoka na pointi zote mbele ya mnyama Simba aliye kwenye kasi ya 4G.

Ofisa Habari wa klabu hiyo Afisa Mteule daraja la pili Constantine Masanja alisema wachezaji wote wako kwenye hali nzuri huku kukiwa hakuna majeruhi yoyote hali inayowapa kiburi cha kuifunga Simba.

"Kikosi kinaendelea na mazoezi chini ya Kocha Shime tukiwa hatuna majeruhi hata mmoja na wachezaji wametuhakikishia ushindi kwahiyo tunasubiri kwa hamu hiyo Jumamosi ifike" alisema Masanja.

Post a Comment

 
Top