BOIPLUS SPORTS BLOG

Paris, UFARANSA
NYOTA wa Real Madrid na timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia FIFA Ballon d'Or 2016  kwa mara ya nne huku akiwabwaga wapinzani wake Lionel Messi na Antoine Griezmann. 

Ronaldo hakuhudhuria sherehe za utoaji wa tuzo hizo kwavile yupo nchini Japan na klabu yake kwenye michuano ya kombe la dunia la klabu.

Baada ya kutangazwa mshindi, Ronaldo alitoa kauli yake akielezea alivyoupokea ushindi huo;

"Ni heshima kubwa kupokea tuzo hii kwa mara ya nne, hisia ni sawa na nilivyotwaa ya kwanza. Ndoto imekuwa kweli tena, sikuwahi kudhani ningekuja kutwaa tuzo hii mara nne, kwahiyo nina furaha sana.
Nawashukuru sana wachezaji wenzangu wa Real Madrid na timu ya Taifa (Ureno) pamoja na watu wote walionisaidia kushinda tuzo hii binafsi.
Mnaweza kufikiri jinsi ninavyojisikia furaha na fahari kupokea mpira huu mzuri na wa kustaajabisha"

Post a Comment

 
Top