BOIPLUS SPORTS BLOG

Akram Msangi, Dar
KIUNGO wa Simba,  James Kotei kutoka Ghana ametua nchini tayari  kusaini mkataba na timu hiyo huku akisema kipa Daniel Agyei alimwambia aje kucheza nchini. 

Akizungumza mara baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere,  Kotei alisema kuwa haifahamu Simba wala watani zao Yanga ila anaamini tu kwamba amekuja kucheza na kila kitu kitaonekana hadharani. 


"Sijawahi kuiona Simba ila Agyei aliniambia nije kwani Simba ni timu nzuri na hata mazingira ni mazuri, Simba nimewaona tu kwenye mechi zao kupitia video,  " alisema Kotei. 

Mchezaji huyo ataungana na wenzake waliopo kambini mjini Morogoro ambapo watarudi Dar es Salaam Jumamosi.


Post a Comment

 
Top