BOIPLUS SPORTS BLOG

Sheila Ally, DAR
KLABU ya Prisons imempa mkataba kocha wa Ndanda, Hamimu Mawazo atakayechukuwa nafasi ya Meja Mstaafu, Abdul Mingange aliyemaliza mkataba wake.

Mingange alisaini mkataba wa miezi sita kuifundisha timu baada ya kocha salum Mayanga kuamua kurudi kwenye ajira yake Mtibwa Sugar.

Habari kutoka ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake jijini Mbeya zinasema kuwa wamekubaliana na Mawazo kuwa ataifundisha timu hiyo kwenye mechi zake za mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom.

"Viongozi wetu walikutana na kujadili juu ya mkataba wa Meja Mingange lakini wameona ni vyema wafanye mabadiliko ya benchi la ufundi ndiyo maana tumemchukuwa Mawazo, tunaamini ni kocha mzuri na atatusaidia," alisema kiongozi huyo.

Prisons tayari ipo kambini huku ikiendelea na usajili wao ambapo hasa wanasaka mshambuliaji atakayerithi nafasi ya Jeremiah Juma ambaye anasumbuliwa na goti na haijulikani lini atarejea uwanjani kwani hata mazoezi mepesi hajaruhusiwa kuanza. Jerry yupo kwao Singida.

Post a Comment

 
Top