BOIPLUS SPORTS BLOG

Madrid, UHISPANIA
IKIUTUMIA uwanja wake wa nyumbani Santiago Bernabeu ambao ulijaza watazamaji 76,894, wababe Real Madrid wameshindwa kuibuka na ushindi dhidi ya Borussia Dortmund ili kujihakikishia nafasi ya kwanza kwenye kundi lao.

Madrid ambayo haijawahi kukosa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Ulaya tangu 1997, ilishuhudia ikilazimishwa sare ya mabao mawili na wageni hao huku bao la kusawazisha likifungwa na Marco Reus dakika ya 89 akimalizia pasi nzuri ya Pierre Aubameyang.

Karim Benzema alikuwa wa kwanza kucheka na nyavu dakika 28 akimalizia kazi nzuri ya Danny Carvajal kabla hajaongeza la pili dakika 53 kwa kichwa kufuatia krosi ya James Rodrigues.

Aubameyang ambaye anasakwa na matajiri hao wa jiji la Madrid, alitumia dakika nane tu kuipatia Dortmund bao la kwanza baada ya Benzema kufunga la pili kwa Madrid.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Szymon Marciniak kutoka Poland, vijana wa Thomas Tuchel walimiliki mpira zaidi ya wenyeji Madrid ambao sasa wamemaliza katika nafasi ya pili.

Haya hapa ni matokeo ya michezo mingine ya ligi ya mabingwa iliyochezwa leo;Post a Comment

 
Top