BOIPLUS SPORTS BLOG

ZIDANE AMWAGIA SIFA BENZEMA
Kocha mkuu wa klabu ya Real Madrid Zinedine Zidane amemsifia mshambuliaji wake Karim Benzema baada ya kufunga goli lake la 50 katika ligi ya mabingwa ya barani ulaya.

Mfaransa huyo aliifungia Madrid mabao mawili dakika ya 28 na 53 katika mchezo dhidi ya Borussia Dortmund ulio malizika kwa sare ya magoli 2-2 na kufikisha idadi hiyo ya mabao.

Zidane alisema "ni vizuri kuendelea kuweka historia huku timu ikipata matokeo mazuri nina furaha Benzema kufikisha magoli 50 katika michuano hii. Kila mechi tunayocheza tunatafuta ushindi ila kuna mechi ambazo matokeo kama haya hutokea".

Benzema imeingia kwenye orodha ya wachezaji watano waliofunga mabao mengi katika michuano hiyo.


AUBAMEYANG AITAKA REAL MADRID
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick Aubameyang amesisistiza kuwa bado ana ndoto za kuchezea  Real Madrid alipokuwa akizungumzia  mchezo kati ya timu hizo uliomalizika kwa sare mabao 2-2. 

Mshambuliaji huyo ameiambia Bein Sport kuwa bado anayafurahia maisha ya Dortmund lakini mustakabali wake wa baadae bado haujulikani. "Najiskia raha sana hapa  ila siku za mbeleni tutaangalia ila sidhani kama nitakuwa hapa msimu ujao".

Aubameyang alifunga na kutoa pasi ya mwisho katika mchezo huo ana mkataba na Dortmund hadi mwaka 2020 huku Wajerumani hao wakiwa tayari kusikiliza ofa ya euro milioni 100 kama ada ya uhamisho wa raia huyo kutoka Gabon.


POCHETTINO ASEMA WATAFANYA MAAJABU UINGEREZA

Kocha wa timu ya Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino 
amesema timu yake imerejea katika kiwango bora baada ya kuifunga Swansea City 5-0 na ushindi wa 3-1 katika ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya CSKA Moscow.

Spurs ilikua nyuma ya goli 1 dhidi Moscow kabla ya kubadilisha matokeo na kushinda mechi hiyo kwa mabao 3-1  kupitia kwa Dele Ali,Harry Kane na bao la kujifunga la golikipa Igor Akinfeev ambapo matokeo hayo yanawapeleka katika mashindano ya Europa ligi baada ya kushika nafasi ya 3 katika msimamo wa kundi lao.

"Ilikua ni muhimu kushinda tulitoka nyuma na kuibuka na ushindi nafikiri tulicheza vizuri na kwa sasa tumeanza kuonyesha kiwango bora" alisema Pochettino.

Post a Comment

 
Top