BOIPLUS SPORTS BLOG

MANCHESTER, Uingereza
ARSENAL wameendelea  kupoteza mechi za ligi ya Uingereza baada ya leo kufugwa mabao 2-1 na Manchester City katika dimba la Etihad.

Wiki iliyopita Arsenal ilifungwa na Everton mabao 2-1 kwenye uwanja wa Godson Park ambapo matokeo ya leo yamewashusha kutoka nafasi ya pili hadi ya nne.

Misimu ya hivi karibuni Arsenal wamekuwa wakipata shida kuelekea kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka kutokana na ratiba ngumu huku wachezaji wake wakipata majeruhi ya mara kwa mara na mambo ambayo pengine yanachangia kupata matokeo mabaya.


Arsenal ndiyo walikuwa wakwanza kupata bao kupitia kwa Theo Walcott dakika ya tano baada ya kupokea pasi ya Alexis Sanchez bao lililodumu hadi kipindi cha kwanza kilipomalizika.

Leroy Sane aliisawazishia City dakika ya 47 baada ya kupokea pasi ya David Silva huku Rahim Sterling alimalizia la pili dakika ya 71 kutokana na kazi nzuri ya Kelvin De Bruyne.

Kwa mara nyingine kiungo Yaya Toure amethibitisha Kocha Pep Guardiola kuwa alikuwa anafanya makosa ya kumuweka benchi baada ya kuikamata vilivyo safu ya kiungo ya Arsenal (kukata umeme) hasa kipindi cha pili iliyopelekea ushindi huo.

Post a Comment

 
Top