BOIPLUS SPORTS BLOG

Akram Msangi, Dar
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom, Yanga chini ya kocha George Lwandamina wamehamishia mazoezi yao Uwanja wa Gymkhana lakini yamekuwa yakifanywa kwa usiri na ulinzi mkubwa jambo ambalo linatafsiriwa kwamba hawataki mbinu zao za uwanjani zijulikane.

BOIPLUS ilifika kwenye viwanja hivyo na kukuta ulinzi mkali sehemu zote huku mashabiki wachache wakichungulia kwa mbali kuona nini kocha huyo mpya anakifundisha kwa mabingwa hao.

Hata hivyo, ilikuwa ni vigumu kwa mtu yoyote kuingia ndani ya uwanjani kushuhudia kwa ukaribu mazoezi hayo yaliyoonekana kuwa na mbinu mpya nyingi kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi ligi kuu ya Vodacom.

Walinzi wa Uwanja huo walipogundua kuwa kuna waandishi wa habari nje ya uzio wa uwanja huo waliwafuata na kuwapa amri ya kuondoka eneo hilo huku wakiwazuia kufanya jambo lolote ikiwemo upigaji picha, waandishi walitii na kuondoka.

Inadaiwa kuwa walinzi hao walipewa agizo na uongozi wa Yanga kuzuia mtu yeyote kuingia uwanjani isipokuwa kwa kibali maalumu kutoka kwa uongozi. Huo ndio utaratibu ambao Yanga wamejiwekea ili kuficha siri zao za mazoezini.

Post a Comment

 
Top