BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu, DAR
KIUNGO mpya wa Yanga, Justine Zulu ataonekana kwa mara ya kwanza uwanjani pale timu yake itakaposhuka katika dimba la Uhuru kumenyana na JKU ya Zanzibar Jumamosi hii kwenye mchezo wa kirafiki.

Yanga ilikuwa imehangaika kwa kipindi kirefu kupata kiungo mkabaji wa kiwango cha juu na sasa wapenzi wa timu hiyo watapa nafasi ya kufahamu kama mzambia huyo ni jibu au la.

Viingilio katika mchezo huo utakaoanza majira ya saa  10 alasiri vitakuwa ni Sh 5,000 kwa mzunguko na Sh 10,000 kwa VIP huku tiketi zitakazotumika zikiwa ni zile za kielektroniki.

Katika hatua nyingine taarifa ya klabu hiyo imesema watautumia mchezo huo kumuaga rasmi kiungo Mbuyu Twite ambaye ameachwa na nafasi yake imechukuliwa na Zulu

Post a Comment

 
Top