BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
NI kama vile wanachama wa Simba wemwambia mfanyabiashara Mohamed Dewji 'Mo' sasa kazi ni kwako baada kupitisha kipengele cha mabadiliko ya mfumo kwenye katiba yao ili kubadili uendeshwaji wake katika mkutano mkuu wa dharura uliofanyika kwenye ukumbi wa Polisi Officers Mess Osterbay jijini Dar es Salaam.

Katiba ya sasa ya klabu hiyo hairuhusu kufanya mabadiliko yoyote ya kiundeshwaji ambapo kwa kupitisha kipengele hicho inamaanisha sasa MO ana nafasi ya kuwekeza hisa kwa asilimia 51 kama mpinzani atakayewekeza zaidi.


Mkutano mkuu uliopita uliofanyika Julai 31 ulipitisha kwa nia moja dhamira ya kuhitaji mabadiliko ya kiundeshwaji ambapo MO alionyesha nia ya kuwekeza hisa hizo kwa ajili ya maendeleo ya klabu.

Aliyekuwa katibu mkuu wa zamani wa klabu hiyo ambaye ni Mwanasheria wa kujitegemea Evodius Mtawala ndiye aliyeongoza mchakato wote wa kupitisha kipengele hicho cha mabadiliko ya katiba huku asilimia 98 ya wanachama waliohudhuria mkutano huo walipiga kura ya ndiyo wakimaanisha kukubali mabadiliko.

Baada ya marekebisho hiyo kupitishwa yatapelekwa kwa Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) kuipitia kabla ya kupelekwa kwa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) ili kuisajili.

Post a Comment

 
Top