BOIPLUS SPORTS BLOG

BROMWICH, Uingereza

MSHAMBULIAJI Zlatan Ibrahimovic ameisaidia Manchester United kuibuka na ushindi mabao 2-0 ugenini dhidi ya West Bromwich Albion mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Hawthorns.

United imepata ushindi wa tatu mfululizo baada ya kuandamwa na sare ambapo sasa wamefikisha pointi 30 sawa na Tottenham Hotspurs lakini wameendelea kubaki nafasi ya sita kutokana na tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.


Ibrahimovic alifunga bao la kwanza dakika ya tano akimalizia mpira wa krosi wa Jesse Lingard upande wa kulia wa uwanja kabla ya kufunga jingine dakika ya 56 akimalizia pasi ya Wayne Rooney.

Matokeo ya mechi nyingine zilizochezwa leo ni

Crystal Palace 0-1 Chelsea
West Ham 0-1 Hull City
Middlesbrough 3-0 Swansea City
Stoke City 2-2 Leicester City
Sunderland 1-0 Watford

Post a Comment

 
Top