BOIPLUS SPORTS BLOG

WENGER ALIMBANIA VIEIRA

Kiungo wa zamani wa timu ya Arsenal Patrick Vieira alitaka kupata nafasi ya kuwaongoza 'Washika bunduki' akiwa kocha lakini Arsene Wenger alimbania nafasi hiyo.

Vieira ambaye aliitumikia klabu hiyo kwa miaka tisa alivunjwa moyo na kocha wake huyo wa zamani kutompatia nafasi hiyo kabla ya kujiunga na kikosi cha vijana cha timu ya Manchester City. Mshindi huyo wa kombe la dunia mwaka 1998 hakuweza pata nafasi hiyo pamoja na kupitia madarasa ya ukocha aliyopitia kocha Wenger.

"Ni kweli baada ya kuitumikia Arsenal kwa miaka tisa mahali ambapo nilicheza kwa ubora nilipenda kupatiwa nafasi ya kuwa kocha kwa bahati mbaya haikuwa hivyo na bahati nzuri nilienda Man City kwa wakati sahihi ila nilivunjwa moyo na Wenger".


MOURINHO AMFAGILIA MKHITARYAN

Baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Zorya kwenye michuano ya Uropa kocha wa Manchestar United Jose Mourinho amemsifia kiungo mshambuliaji Henrikh Mkhitaryan kwa uwezo alioonyesha katika ushindi huo wa ugenini.

Mourinho alimsifia Mkhitaryan baada ya kufunga bao zuri kwa kuwapinga chenga mabeki kadhaa kabla ya kufunga  katika dimba la Stadion Chornomorets mjini Kiev.

Mkhitaryan amechukua miezi kadhaa  kuwazoea wenzake akiwa dimbani mara baada ya kusajaliwa na Mashetani hao akitokea Borussia Dortmund ya Ujerumani mwezi Julai.

"Ni jasiri sana alijitoa kupigana na hali ya kuzoea haraka na anafanya vizuri sasa alifanya mazoezi kwa nguvu zote na kipaji alichojaliwa tulijua tunachokinunua kwa sasa anacheza vizuri katika mechi zote"alisema Mourinho.


RONALDO ANATII SHERIA BILA SHURUTI.

Moja ya kampuni ya mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo imetoa uthibitisho kuwa nyota huyo hutii sheria  bila shuruti kwa kulipa kodi zake kama ipasavyo.

Kampuni hiyo inayoitwa Gestitufe imetoa uthibitisho wa staa huyo kuwa amelipa kodi zote kwa usahihi na kutokwepa hata moja ambapo nyota huyo ameshutumiwa kutolipa kodi kama wachezaji wengine Lionel Messi,Neymar na Javier Mascherano. 

Ronaldo anamiliki mali mbali mbali zenye  thamani ya Euro milioni 203 ambazo aliziweka wazi.

Nyota huyo aliwasiliana na wakala wa kodi nchini Hispania kuhusu aseti zote anazomiliki zikiwa zimeorodheshwa katika nyaraka moja.

Post a Comment

 
Top