BOIPLUS SPORTS BLOG

Akram Msangi, DAR
 Mpiga picha wa siku nyingi Mpoki Bukuku aliyefariki juzi kwa ajali ya gari ameagwa rasmi leo nyumbani kwake Tabata Kimanga kabla ya kuanza safari ya kwenda kuzikwa mkoani Dodoma. Pichani ni mjane wa marehemu akiubusu mwili kama ishara ya kumuaga

 Msanii wa filamu Steve Nyerere akielekea kuaga mwili wa marehemu

 Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na michezo, Mh. Nape Nnauye (katikati) alishiriki shughuli hiyo pamoja na Mwenyekiti wa kambi ya Upinzani Bungeni Mh. Freeman Mbowe (kulia) na mbunge wa Ubungo Mh. Said Kubenea

Afsa Habari wa TFF, Alfred Lukas aliwaongoza waandishi wa habari  za michezo katika kumuaga marehemu Bukuku

 Mh. Nape akitoa hotuba fupi kabla zoezi za kuuaga mwili halijaanza

Katika sanduku hili ndimo umewekwa mwili wa marehem Bukuku

Hapa sanduku lililobeba mwili wa marehemu Bukuku likipakiwa kwenye gari tayari kwa kuanza safari.


Menejimenti ya BOIPLUS MEDIA inawapa pole wafiwa wote.
Bwana alitoa na bwana ametwaa, jina la bwana lihimidiwe, AMIN.

Post a Comment

 
Top