BOIPLUS SPORTS BLOG

Mpigapicha Wetu
 Kikosi cha Yanga kinaendelea na mazoezi yake chini ya kocha George Lwandamina katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. Kiungo mpya wa timu hiyo Justine Zulu (wapi kushoto) amejiunga rasmi na wenzake leo.


 Kivutio kikubwa katika mazoezi hayo ni jinsi nyota wa kikosi hicho wanavyopambana kwa nguvu. Unaweza kudhani ni mechi, hali hii ni kutokana na ushindani mkubwa wa namba uliopo kikosini hapo. Pichani ni mshambuliaji Malimi Busungu akimfungisha tela Oscar Joshua huku Obrey Chirwa na Juma Mahadhi wakisubiri kutoa msaada.


Ngoma ya moto, acha tupoze.....walinzi Haji Mwinyi na Nadir Haroub 'Canavaro' aliyekaa chini wakijipoza kwa maji baada ya shughuli nzito.

 Busungu vs Matheo Anthony


 Kocha msaidizi Juma Mwambusi akitoa maelekezo kwa vijana wake


 Beki Kelvin Yondan akianzisha mpira kwa kuupiga mbele


Chirwa akimiliki mpira mbele ya Canavaro

Post a Comment

 
Top