BOIPLUS SPORTS BLOG

Akram Msangi, DAR
Nyota wa mchezo wa jana, Haruna Niyonzima akiwania mpira na nahodha wa JKT Ruvu Michael Aidan

  Simon Msuva alifunga mabao mawili huku pia akisababisha moja ambalo beki Aidan alijifunga katika harakati za kuokoa krosi ya nyota huyo

Hatari langoni mwa Ruvu, vijana hao wa Mlandizi walishindwa kabisa kuwazuia Yanga hasa katika kipindi cha pili

Msuva, Niyonzima na Deus Kaseke wakicheza dansi kufurahia bao la kwanza dhidi ya Ruvu

 Kaseke ambaye alisaidia upatikanaji wa bao la pili akitafuta mbinu za kumtoka mlinzi wa Ruvu

Niyonzima 'on fire'

 Msuva akimtoka Edward Joseph wa Ruvu Juma Abdul alikosa mechi kadhaa za mwisho katika mzunguko wa kwanza kutokana na majeruhi, sasa amerejea uwanjani na jana alifanikiwa kuonyesha uwezo mkubwa

Naftal Nashon (24) na Edward Charles (27) wakimchunga Niyonzima asilete madhara katila lango lao

Donald Ngoma akimiliki mpira

Msuva 'on air'

Katika mchezo wa jana kocha George Lwandamina hakuwa akiinuka kutoa maelekezo, badala yake kocha msaidizi Juma Mwambusi na Mshauri wa Ufundi, Noel Mwandila ndio waliokuwa wakitoa maelekezo kwa wachezaji

 Ni kama vile anasema "Kijana kuwa makini usije ukanifunika".... Ngoma akimpongeza MsuvaKiungo Justine Zulu akitazama mchezo huo akiwa jukwaani kufuatia kukosa kibali cha kufanyia kazi nchini

Mashabiki wa Yanga wakicheza kwa furaha

Kocha wa Ruvu Bakari Shime akiwa ameduwaa baada ya timu yake kupoteza mwelekeo uwanjani

Benchi la Ufundi la Yanga

Wachezaji wa akiba wa Ruvu 

Wachezaji wa akiba wa Yanga

Post a Comment

 
Top