BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
Mzee Hamis Kilomoni

DANADANA za mabadiliko ndani ya klabu ya Simba zimeingia hatua nyingine baada ya leo baraza la wadhamini kutangaza kuwa limemtaka mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kusimamisha mkutano wa dharura wa mabadiliko ya katiba uliopangwa kufanyika Disemba 11 kutokana na wao kutoshirikishwa chochote kama wenye mali.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa baraza hilo Mzee Hamisi Kilomoni alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mustakabali wa klabu hiyo akisema inaweza kuleta mpasuko ambao pia unaweza ukaleta madhara makubwa kiusalama.

Kilomoni alisema wamepokea barua kutoka kwa wanachama wa klabu hiyo wakilalamikia mkutano huo ambapo nakala za barua zimefika hadi kwa Rais John Magufuli, Baraza la Michezo (BMT) pamoja na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) ambapo kwa kuliangalia suala hilo kwa mapana yake wakaiomba Serikali kusimamisha mkutano huo.

"Hapa kuna barua nyingi kutoka kwa wanachama kuomba kusitisha mkutano huo, mpaka kufikia kupeleka barua kwa Rais wa nchi ujue hilo sio suala dogo sisi kama wenye klabu tumeamua kumuomba Mkuu wa mkoa kuusimamisha ili isije ikatokea balaa zaidi," alisema Kilomoni.Aidha Mzee Kilomoni amesema bado yeye yupo kwenye orodha ya wadhamini wanne wa klabu hiyo baada ya kupinga kuenguliwa kwenye mkutano mkuu wa wanachama uliofanyika Agosti mwaka 2014.

"Hii hapa barua kutoka RITA iliyotolewa Agosti 12 mwaka huu ikianisha majina ya wadhamini wa klabu ya Simba ambao ni Abdul Wahab Abas, Ally Sykes (marehemu), Ramesh Patel na mimi," alisema nyota huyo za wamani wa Simba.

Post a Comment

 
Top