BOIPLUS SPORTS BLOG

Akram Msangi, DAR
 STRAIKA mpya wa Simba aliyesajiliwa kutoka Stand United, Pastory Athanas leo amecheza mechi yake ya kwanza akiwa na kikosi cha wekundu hao.

 Uwezo mkubwa aliouonyesha Pastory uliwashawishi mashabiki wengi waliohudhuria katika dimba la Uhuru jioni ya leo huku wengine wakishindwa kujizuia na kukiri kuwa "Simba imelamba dume"

 Pastory alikuwa mwiba mkali kwa walinzi wa Ruvu ambao baadaye waliamua kuanza kumchezea 'undava' ili kumtuliza

 Mshambuliaji huyo mwenye nguvu na kasi ndiye aliyepiga krosi iliyozaa bao pekee la Simba lillowekwa nyavuni na Mzamiru Yassin

 Hapa Pastory alikuwa anajaribu  'kusepa na kijiji'

Pastory akimpongeza Mzamiru

Post a Comment

 
Top