BOIPLUS SPORTS BLOG


Kiungo mpya wa Yanga kutoka Zesco ya Zambia, Justine Zulu akisaini mkataba wa miaka miwili kuwatumikia wababe hao wa mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar es Salaam.

Usajili wa Zulu ni ishara kwamba Yanga wanapaswa kuachana na mchezaji mmoja wa kimataifa ili kukidhi kanuni ya ligi kuu inayozitaka timu kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi saba.

Wachezaji wa kimataifa ndani ya Yanga ni beki Vicent Bossou, viungo Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima na Thaban Kamusoko na washambuliaji Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Obrey Chirwa.

Post a Comment

 
Top