BOIPLUS SPORTS BLOG

LEICESTERSHIRE, Uingereza
KOCHA mkuu wa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza Leicester City Muitaliano Claudio Ranieri 'Tinkerman' ametanabaisha wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu sio chanzo cha matokeo mabaya yanayowakuta kwa sasa.

Ranieri amekataa kabisa kuwalaumu wachezaji kama Ahmed Mussa, Islam Slimani na wengine waliosajiliwa klabuni hapo msimu huu ili kuongeza nguvu katika kugombania mataji mbalimbali kwakua bado hawajazoea mikikimikiki ya ligi hiyo.

City ipo nafasi ya 14 katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza baada ya mechi 13 huku wakiwa pointi mbili zaidi ya zile zilizopo kwenye nafasi ya kushuka daraja licha ya kumsajili kwa  gharama kubwa ya pauni 30 milioni  Slimani akitokea CP Sporting ya Ureno.

Leicester City wamefanya vizuri katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya baada ya kufuzu hatua ya 16 bora ikiwa wanashiriki kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake.

Ranieri alinukuliwa akisema "Usajili ulikuwa mzuri na nina furaha nao ila sio kila mchezaji atakayesajiliwa ataanza kuonyesha makali yake, kama mnakumbuka Mahrez (Riyard) alianza kufanya vizuri msimu wake wa pili klabuni baada ya miezi sita au saba sasa sijui hawa tuliowasajili watachukua muda gani, ukiangalia msimu uliopita na huu ni wazi tunakosa kitu fulani ingawa nguvu ni ile ile."

Leicester inategemewa kumsajili kiungo wa KRC Genk ya Ubelgiji Wilfred Ndidi ingawa kocha huyo hajathibitisha fununu hizo.

Post a Comment

 
Top