BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu
DIRISHA dogo la usajili limefungwa jana usiku huku kiungo mkongwe wa Mbeya City, Ramadhan Chombo 'Redondo' akitupiwa virago pamoja na wenzake saba.

Wengine waliotupiwa virago ni Meshack Samwel, Peter Mwangosi, Michael Kerenge, Mackyada Franco, Issa Nelson, Salvatory Nkulula, Hemedy Murutabose wakati Joseph Mahundi ambaye alikuwa anahitajika kikosini humo alisaini Azam baada ya mkataba wake kumalizika.

City imetangaza nyota wapya 11 ambao ni Mrisho Ngassa, Juma Seif Kijiko, Hood Mayanja, Tito Okello, Zahor Pazzi, Hussein Salum, Otong William, Raphael Bryson, Daniel Joram, Sameer Abeid na Majaliwa Mbanga.

Akizungumza mara baada ya kumalizana na Mbeya City kwa mkataba wa mwaka mmoja, Ngassa ambaye alipewa jezi namba 10 iliyokuwa inavaliwa na Mahundi, alisema kuwa amekwenda City kwa lengo moja la kuisaidia timu hiyo kufanya vizuri kwenye mechi za mzunguko wa pili wa ligi.

"Najua kuna maneno na minong'ono mingi kuhusu uwezo wangu, muda si mrefu yataisha kwa sababu najua nini nataka kufanya, soka ndiyo maisha yangu, naomba watu wote walio nyuma ya timu hii waniunge mkono nina uhakika tutakuwa na majibu mazuri mwisho wa msimu," alisema Ngassa.

Post a Comment

 
Top