BOIPLUS SPORTS BLOGMSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameifungia klabu yake hat- trick katika ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Kashima Antlers, Japan

Ushindi huo wa 4-2 umeifanya Real Madrid kunyakua taji la hilo na klabu duniani. Real Madrid ilitumia dakika 120 kupata ushindi huo mara baada ya kwenda sare ya 2-2 hadi dakika 90 za mchezo.

Katika karatasi ilionekana Kashima Antlers watapoteza mchezo huo kirahisi mbele ya miamba hiyo ya Uhispania. Kashima wakiwa klabu ya kwanza kutoka Japan kufika fainali ya ngazi ya klabu duniani

Mbele ya mashabiki 68,000 katika dimba la Nissan Stadium huko Yokohama Real Madrid wameweza kutwaa taji hilo kupitia wafungaji wake Karim Benzema aliyeifungia goli la kwanza na hat- trick ya Ronaldo huku Kashima wakipata mabao kupitia Shibasaki aliyefunga mabao mawili

Michuano hiyo imefikia tamati ikishuhudia Ronaldo akitwaa tuzo ya mpira wa dhahabu huku kiungo Luka Modric akipata tuzo ya fedha na Shibasaki akitwaa shaba.

Post a Comment

 
Top