BOIPLUS SPORTS BLOG

ZÜRICH, Uswis
NYOTA watatu wanaokipiga kwenye ligi kuu nchini Hispania Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Antoine Griezman wameingia kwenye tatu bora ya kinyang'anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d'Or.

Messi ndiye anayeongoza kwa kunyakua tuzo hiyo baada kuchukua mara tano huku mpinzani wake mkubwa katika medani ya soka kwa sasa Ronaldo akichukua mara tatu.

Ronaldo anapewa nafasi kubwa ya kunyakua tuzo hiyo baada ya kuisaidia nchi yake ya Ureno kunyakua ubingwa wa Euro 2016 pia kuisaidia timu yake ya Real Madrid kuchukua klabu bingwa barani Ulaya.


Griezmann hapewi nafasi kubwa ya kuibuka kidedea kwenye kinyang'anyiro hicho baada ya kupoteza fainali mbili ya Euro ambayo Taifa lake la Ufaransa ilifungwa na Ureno na timu yake ya Atletico Madrid wakipoteza mbele ya majirani zao Real Madrid kwenye mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya licha ya kuchukua tuzo ya mfungaji bora wa michuano ya mataifa ya Ulaya ambayo yalifanyika nchini kwao.

Fainali za tuzo ya mchezaji bora wa dunia zinatafanyika Januari 9 mwakani jijini London.

Post a Comment

 
Top