BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar

HATIMAYE winga wa Azam FC Farid Mussa sasa ataondoka mwezi ujao, Januari kuelekea Hispania tayari kujiunga na klabu ya Tenerife inayoshiriki ligi daraja la pili baada ya kila kitu kukamilika.

Azam ilituma hati yake ya uhamisho ya kimataifa (ITC) kwa klabu hiyo lakini upatikanaji wa kibali cha kufanya kazi nchini Hispania ndio uliochelewesha dili hilo lakini sasa kila kitu kipo sawa na nyota huyo ataondoka mwezi ujao.

Ofisa Habari wa klabu hiyo, Jaffar Iddi, alisema kumekuwa na taarifa za upotoshwaji kuwa uongozi wao ndiyo chanzo cha kuchelewesha dili hilo kitu ambacho sio kweli lakini sasa mambo yako vizuri na nyota huyo atasafiri.

"Kuna taarifa kuwa uongozi ulikuwa unambania Farid kuondoka sio kweli kilichokuwa kinachelewesha ni kibali cha kazi nchini Hispania. Sasa kama sisi hatutaki aondoke mbona tushatuma ITC yake," alihoji Maganga.

Kwa upande wake Faridi ameushukuru Uongozi wa klabu hiyo hasa Meneja wa timu hiyo Abdul Mohamed kwa kusimamia suala hilo hadi kufikia hapo huku akiwataka Watanzania kumuombea ili akafanikiwe.

"Namshukuru Mungu hadi kufikia leo safari ipo mbioni kukamilika ila niwatoe hofu watu waliokuwa wakiamini kuwa uongozi wangu ndio uliokuwa sababu ya kuchelewesha dili langu taarifa hizo sio za kweli. Uongozi ulikuwa bega kwa bega na mimi hadi kufikia leo," alisema Faridi.

Post a Comment

 
Top