BOIPLUS SPORTS BLOG


STRAIKA wa KRC Genk na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Mbwana Samatta usiku wa leo ameisaidia klabu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 ugenini dhidi ya Waasland-Beveren.

Samatta ambaye alikumbwa na ukame wa mabao kwa zaidi ya miezi miwili alifunga bao lake la kwanza dakika ya 15 kabla hajaongeza la pili dakika mbili kabla timu hazijaenda mapumziko katika mchezo huo wa kombe la ligi almaarufu 'Crocky Cup'.

Kipindi cha pili Genk walioonekana kupania kurejesha heshima baada ya juma lililopita kuadhibiwa mabao 6-0 dhidi ya Oostende, walijipatia bao la tatu kupitia kwa Mnaijeria Wilfred Ndidi dakika ya 80.

Wenyeji Waasland walifunga bao la kufutia machozi dakika ya 89 mfungaji akiwa ni Zinho Gano.

Samatta aliyewasumbua vilivyo walinzi wa Waasland alitolewa katika dakika za nyongeza huku nafasi yake ikichukuliwa na Nikos Karelis.

Post a Comment

 
Top