BOIPLUS SPORTS BLOG

Akram Msangi, Dar
 BAADA ya mshambuliaji Amissi Tambwe kuisawazishia Yanga bao dhidi ya African Lyon katika dakika ya 74, Obrey Chirwa alikimbia na kwenda kuuchukua mpira nyavuni ili uanze haraka. 

 Tukio hilo lilisababisha kipa wa Lyon Youthe Jehu atake kumpora mpira Chirwa jambo ambalo lilizua sintofahamu ndani ya nyavu za lango la Simba hao wa Kiafrika huku beki Hamad Waziri akiingilia kati kupambana na Chirwa.

 Kamera ya BOIPLUS iliyokuwa imetegwa nyuma ya lango hilo ilifanikiwa kunasa matukio yote hadi watatu hao walipoamuliwa.


Post a Comment

 
Top