BOIPLUS SPORTS BLOG


INTER KUIPIKU EVERTON KWA SCHNEIDERLIN

MIAMBA ya soka nchini Italia Inter Milan imeingia katika kinyang'anyiro cha kumnasa kiungo mkabaji wa Manchester United Morgan Schneiderlin ambaye hana nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Huenda nyakati mbaya zikaisha kwa kiungo huyo mara baada ya taarifa ya kuhitajika na klabu hizo huku Everton  wakiwa mstari wa mbele kumnasa mwezi Januari na Milan nao wakiwa katika mazungumzo ya kuhitaji huduma yake. 

Gazzetta dello Sport limeripoti kuwa kocha mkuu wa Inter Stefano Pioli anahitaji kiungo mkabaji na Schneiderlin ndiyo chaguo lake la kwanza  lakini dili hilo likibuma watamgeukia kiungo wa Chelsea Mikel Obi.


 INTER, NAPOLI NA ROMA ZAMNYATIA CLICHY

Beki wa kushoto wa Manchester City Gael Clichy anatakiwa na miamba ya soka nchini Italia baada ya kumaliza mkataba wake kwa mujibu wa  Mundo Deportivo.

Beki huyo ambae mkataba wake unaisha mwakani amezivutia klabu za Napoli, Inter Milan na As Roma zinazoshiriki ligi ya Italia.

Klabu hizo huenda zikatuma ofa mapema Januari katika usajili wa dirisha dogo kabla ya kusubiri mkataba wake uishe mwezi wa sita.


BAYERN WAMTAKA DIER

Mabingwa wa ligi ya Ujerumani Bayern Munich wanamtolea macho kiungo mkabaji wa Tottenham Hotspurs Eric Dier baada ya klabu hiyo kutafuta kiungo wa kuboresha kikosi chao.

Bayern imeungana na klabu za  Chelsea na Manchester City katika kinyang'anyiro cha kumnasa Dier na inasemekana  kiungo huyo hana furaha tena klabuni  hapo kutokana na kupungua kwa dakika za kucheza chini ya kocha Mauricio Pochettino

Kocha Spurs amekanusha taarifa hiyo akisema "Najua kumekuwa na fununu nyingi ila Dier ni mchezaji wetu asilimia 100 na tayari kasaini mkataba mpya kuonyesha yupo tayari kuitumikia klabu hii kwa muda mrefu zaidi".


Post a Comment

 
Top