BOIPLUS SPORTS BLOG

www.boiplus.blogspot.com
RODRIGUEZ KUTIMKIA UINGEREZA

Kiungo mshambuliaji wa Real Madrid James Rodriguez huenda akatimkia katika ligi kuu  nchini Uingereza baada ya kukiri kuwa hana uhakika wa kubaki na miamba hiyo ya Hispania. 

Raia huyo Colombia huyo ambae anapata nafasi ndogo ya kucheza chini ya kocha Zinedine Zidane  ameamua kuangalia ofa kutoka klabu mbali mbali  nchini Uingereza.

Miongoni mwa klabu zinazomuhtaji ni Manchester United,Arsenal na Chelsea ambao wapo katika mstari wa mbele kumpata kiungo huyo mshambuliaji.

"Ningependa kucheza zaidi kuna ofa zimekuja kwangu nahisi ni muda muafaka wa kufanya maamuzi sina uhakika wa kubakia Madrid" alisema Rodriguez.

LUKAKU AJIFUNGA ZAIDI EVERTON

Mshambuliaji  wa Everton Romelu Lukaku huenda akasaini mkataba mpya klabuni hapo mara baada ya klabu hiyo kuridhika na huduma yake.

Lukaku ambae mkataba wake wa sasa anapokea kitita cha paundi  75,000 kwa wiki ataongezwa hadi  kufikia paundi 100,000 kwa wiki ambapo kwa sasa ana mkataba na Everton hadi 2019.

Mkataba huo mpya utakuwa ni kujikinga na ofa mbalimbali ambazo mshambuliaji huyo alikuwa anapokea ili kutimka klabuni hapo. Tottenham na Chelsea ndiyo  zipo  karibu kuwania saini ya raia huyo wa Ubelgiji.

CONTE KUJIUNGA TENA NA VIDAL

Kocha wa Chelsea  Antonio Conte amemuweka Arturo Vidal katika orodha ya wachezaji anaowataka wajiunge nae  Stamford Bridge.

Kiungo huyo anayecheza klabu ya  Bayern Munich amekua katika orodha hiyo ya Conte huku Chelsea ikiandaa ofa ya paundi milioni 42 kupata huduma yake.

Vidal yupo tayari kuhama Bayern katika  majira ya joto mwezi Juni mwakani kujiunga na kocha wake aliemfundisha kwa miaka mitatu wakiwa Juventus.

WEIGL ASAINI MKATABA MPYA DORTMUND

Klabu ya Borussia Dortmund imefikia maamuzi ya kumuongezea mkataba kiungo Mjerumani Julian Weigl hadi 2021.

Weigl amekua akihusishwa na miamba ya soka ya Hispania Real Madrid ili  kumsaidia Casemiro katika nafasi ya kiungo mkabaji. Mkataba huo mpya utamfanya Weigl awe na miaka 5 zaidi klabuni hapo.

Mkataba huo unaifanya Madrid kuachana na kiungo huyo au kuandaa ofa kubwa zaidi  kuishawishi Dortmund wamuuze kiungo huyo.

SIGURDSSON KUTIMKIA ROMA

Mchezaji wa timu ya taifa ya Iceland na klabu ya Swansea Glyfi Sigurdsson huenda akatimkia As Roma ya Italia katika dirisha dogo la usajili mwezi ujao.

Daily Express wameripoti kuwa  Roma wameonyesha nia ya kumtaka kiungo huyo mshambuliaji ambaye klabu yake ipo katika nafasi za kushuka daraja katika ligi kuu nchini Uingereza.

Sigurdsson huenda akaifikiria ofa hiyo ili aweze  kucheza klabu bingwa barani Ulaya huku akikwepa kubakia Swansea na kushuka daraja kutokana na nafasi yao katika msimamo wa ligi.

Kocha Bob Bradley huenda akawawekea ngumu Roma katika kumpata kiungo huyo ili aweze kubakia klabuni hapo kusaidia kujitoa katika nafasi mbaya ya kushuka daraja.

Post a Comment

 
Top