BOIPLUS SPORTS BLOG

www.boiplus.blogspot.com
MADRID WAMTAKA MESSI

Mshambuliaji wa Barcelona Lionel  Messi amehusishwa na kujiunga na Real Madrid baada ya taarifa kutoka kwa nyota huyo kukataa kusaini mkataba mpya.

Rais wa Real Madrid Florentino Perez  inasemekana anategemea kusajili wachezaji wenye majina makubwa  majira ya joto na mmoja wao akiwa Messi kutokana na kukataa kusaini mkataba mpya.

Mkataba wa Messi kwa sasa una thamani kati ya paundi milioni 150 hadi 200. Madrid  itawalazimu watoe kiasi hicho cha pesa na Messi pia akubali kujiunga na miamba hiyo. 


BALOTELI KUREJEA UINGEREZA

Mshambuliaji Mario Balotelli huenda akajiunga na klabu inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza  baada ya kurudi katika kiwango kizuri uwanjani.

Wakala wa mshambuliaji huyo Mino Raiola alisema wamefanya  mazungumzo na klabu mbali mbali zinazoshiriki ligi kuu nchini Uingereza alipokuwa akiongea na Talk Sport.

Raiola alisema "tumefanya mazungumzo na klabu mbalimbali zinazoshiriki Ligi kuu Uingereza na ni matumaini yangu Balotelli atarejea katika ligi kuu Uingereza".LINDELOF KUTUA MAN UTD

Beki wa kati wa timu ya Benifica Victor Lindelof hatimaye anakaribia kutua Manchester United baada ya kumfatilia kwa miezi miwili mpaka sasa.

Viongozi wa Benfica walionekana katika jiji la Manchester wakiwa wameenda kukamilisha dili la uhamisho wa beki huyo lenye thamani ya paundi milioni 42 katika dirisha la usajili la mwezi Januari. 

Lindelof atajiunga na United wiki ijayo baada ya dili hilo kukamilika ambapo kocha Jose Mourinho amekuwa akimtaka beki huyo ili  kuziba pengo atakaloliacha Eric Bailly ambaye atakua na majukumu na timu ya taifa katika michuano ya kombe la mataifa Afrika.MAN CITY WANYATIA VAN DIJK

Klabu ya Man City imeanza mazungumzo na Southampton kwa ajili ya kutaka kumsajili beki wa kati Virgil Van Dijk.

ESPN wanataarifu kuwa pamoja na mazungumzo kuanza Man City wapo tayari kutoa dau la paundi milioni 50 ili waweze kupata saini ya Mholanzi huyo na kuwapiku Chelsea na Liverpool ambao pia wapo katika kinyang'anyiro hicho.

Kocha Pep Guardiola amekuwa akimfuatilia Van Dijk na kuridhishwa na uwezo wake hivyo kumfanya aamini  ndiyo mtu sahihi wa kuboresha safu yake ya ulinzi baada ya John Stones kusua sua tofauti na matarajio ya washabiki wengi wa City.


JUVENTUS WAMTAMANI JAMES RODRIGUEZ

Klabu ya Juventus imejiunga katika kinyang'anyiro cha kutaka kumsajili kiungo mshambuliaji wa Real Madrid James Rodriguez baada ya ya kuhusishwa na klabu mbalimbali za ligi kuu nchini Uingereza.

Rodriguez ambae amekiri kuanza kuzifikiria ofa zilizomfikia amekuwa na wakati mgumu baada ya kupata nafasi ndogo ya kucheza chini ya kocha Zinedine Zidane.

Meneja wa Juventus Guiseppe Marotta akiongea na La Gazzetta dello Sport alisema "Inategemea na malengo yetu katika usajili tunatakiwa kuheshimu mahesabu yetu ila tungependa kujiweka katika nafasi ya klabu bora duniani
Kwa kusajili wachezaji wakubwa kama James".TORINO KUMALIZIA DILI LA HART

Golikipa wa Manchester City ambaye yupo kwa mkopo Torino Joe Hart huenda akasaini mkataba klabuni hapo moja kwa moja mara baada ya klabu hiyo kuridhishwa huduma yake akiwa katika usajili wa mkopo.

Hart amekuwa akihusishwa na Liverpool ambapo  Torino imeona bora kumalizana na mlinda mlango huyo na kumkataka maini Kocha Jurgen Kloop ambaye anamtolea macho. 

City imesajili golikipa mpya Claudio Bravo na hajawa na msimu mzuri na amekua akifanya makosa kadhaa yaliyoigharimu timu hiyo.

Post a Comment

 
Top