BOIPLUS SPORTS BLOG

www.boiplus.blogspot.com
HAZARD NA JAMES RODRIGUEZ KUPISHANA

Miamba ya soka ya Hispania Real Madrid ipo katika mipango ya kumzuia James Rodriguez asiondoke mwezi Januari ili waweze kumtumia katika dili la kumvuta Eden Hazard na golikipa Thibaut Courtois.

Chelsea ambao wanajiandaa kutoa dau la paundi milioni 63 ili kumpata kiungo mshambuliaji huyo watapata wakati mgumu kwani Madrid inamuhitaji Hazard ambaye ni tegemezi ndani ya vijana hao wa Antonio Conte.

Kutokana na kila upande kutaka mchezaji kwa mwenzake hivyo inasemekana kufanya dili ya kubadilishana wachezaji litakalowahusu Rodriguez, Courtois na Hazard.


SEVILLA WAMTAKA MARTIAL

Mshambuliaji wa Manchester United Antonio Martial huenda akajiunga na Sevilla mwezi Januari baada ya klabu hiyo kuonesha nia ya kutaka kumsajili.

Gazeti la Express la Uingereza limetaarifu kuwa Sevilla wapo tayari kumchukua Martial kwa mkopo wa miezi 6 katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari.

Martial angependa kupata nafasi zaidi ya kucheza kwani chini ya kocha Jose Mourinho nafasi yake imepungua zaidi dimbani.

Sevilla wanafikiria  kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ili kujihakikishia nafasi za juu zaidi katika ligi kuu nchini Hispania huku wawakilishi wa Martial wakiwa wamefanya mazungumzo na viongozi wa klabu hiyo mwezi uliopita.


JUVENTUS NA MILAN ZAMNYATIA SCHNEIDERLIN

Kiungo aliyekosa nafasi katika klabu ya Manchester United Morgan Schneiderlin amehusishwa na kutaka kujiunga na klabu za Inter Milan na Juventus za nchini Italia.

Schneiderlin anafuatiliwa kwa karibu zaidi na klabu hizo baada ya kuwa na wakati mgumu klabuni hapo katika miezi 18 aliyokuwepo kwa Mashetani hao.

Kocha mkuu wa United Jose Mourinho alikiri kuwa kama kutakua na ofa yoyote ambayo Schneiderlin itamvutia na bodi ya klabu hiyo ikakukubali basi kiungo huyo ataruhusiwa kuondoka klabuni hapo.


SPURS WAMRUDIA  MEYER

Klabu ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza imeamua kurejesha jitihada zake za kumsajili kiungo wa Schalke 04 Max Meyer.

Tangu majira ya joto yaliopita Spurs wamekuwa wakihusishwa na kiungo huyo na sasa wameamua kurejesha jitihada hizo za kumsajili mwezi Januari katika dirisha dogo la usajili.

Meyer Mwenye umri wa miaka 21 amekuwa mmoja wa wachezaji hodari kwa upande wa Schalke  iliopelekea kocha Mauricio Pochettino kuvutiwa na huduma zake

Schalke 04 imetoa kauli kuwa kiungo huyo hatoruhusiwa kuondoka mpaka pale Spurs au klabu yoyote inayomtaka kutoa kitita cha paundi milioni 30 kama ada ya uhamisho ya kiungo huyo.


UNITED NA CITY WAPIGANA VIKUMBO KWA SANDRO

Beki wa kushoto wa Juventus Alex Sandro amehusishwa na kutaka kujiunga na  klabu za Manchester City na Manchester United mwezi Januari.

Sandro ambaye kwa sasa ni majeruhi amehusishwa na klabu hizo kutokana na mabeki wao wa kushoto kushindwa kufanya hivyo kumuhitaji raia huyo wa Brazil anayetumia zaidi nguvu uwanjani.


BACCA KUBAKIA  MILAN

Mshambuliaji wa AC Milan Carlos Bacca ambaye amekuwa akihusishwa na kujiunga na klabu mbalimbali barani Ulaya ameamua kubaki kwa miamba hiyo ya Italia.

Suso Fernandez ambae anacheza nae  Milan alisema “nafikiri hivyo nilimuuliza Bacca ukaniambia ana furaha klabuni hapa na najua atabakia hapa ila  katika soka kila kitu hubadilika kulingana na nyakati ila itakukuwa vyema akibaki nasi".

Bacca amehusishwa na klabu kama Barcelona ambao waliokua mstari wa mbele kumnasa huku  Sevilla,Chelsea na Real Madrid wao wakionesha nia ya kumpata.

Imeandaliwa na Abra David kwa msaada wa mitandao

Post a Comment

 
Top